Sat. May 16th, 2026

Na Timoth Anderson

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Elimu,Utamaduni na Michezo imeridhishwa na utekelezaji na usimamizi wa programmu na miradi mbalimbali inayotekelezwa na Taasisi ya Elimu ya watu Wazima nchini.

programu hizo ni elimu changamani baada ya msingi (IPPE),mpango wa elimu changamani kwa vijana walio nje ya mfumo rasmi (IPOSA) mradi wa kuimarisha elimu ya sekondari kwa njia mbadala (SEQUIP-AEP)

Makamau Mwenyekiti wa kamati hiyo,Mh Mussa Sima amesema kamati yake imeridhishwa na shughuli za utekelezaji wa mipango na programu za Elimu na mpango inayolenga kuwarejesha vijana walikosa masomo wanarejeshwa katika katika mfumo rasmi.

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Mh Adolf Mkenda amesema serikali awamu ya sita itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuboresha sekta ya Elimu kwa njia mbadala na kuboresha mazingira ya kujifunza na kuifunzia.