Sat. May 16th, 2026

Kamishna wa Uhifadhi, Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA), Bw. Abdul-Razaq Badru ameungana na viongozi wengine walioteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungaano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kula Kiapo cha Maadili katika hafla iliyofanyia Ikulu Chamwino Dodoma.

Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemtaka Kamishna Badru kusimamia kikamilifu shughuli za Uhifadhi, kulinda Ikolojia, Uwekezaji na Maendeleo ya Jamii. 

Dkt Samia amesema Ngorongoro ni Urithi wa Dunia hivyo ni lazima ilindwe kuhakikisha kwamba ikolojia yake inaimarishwa na kulinda rasilimali zilizopo na kuhakikisha kuwa  umaarufu wake haupotei. 

Amesema ana matumaini makubwa na Kamishna Badru kutumia maarifa yake, ujuzi na uzoefu wake katika kuisimamia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.

Rais Samia  alimteua Bw. Abdul-Razaq Badru kuwa Kamishana wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro tarehe 26 Mei, 2025.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *