Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh Dkt Samia Suluhu Hassan ameamua kuweka utaratibu wa kuwasilikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabiri wananchi bila ya ubaguzi katika ofisi ndogo ya Chama cha Mapinduzi Lumumba, ofisi kuu ya Dodoma na Zanzibar kila mwisho wa mwezi ikiwa ni kuenzi jitihada za hayati Rais Mstaafu wa awamu ya pili,Mh Ali Hassan Mwinyi.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi,ndugu Paul Makonda amebainisha utaratibu huo wakati alipokuwa akitoa tathimini ya ziara yake katika mikoa 23 ya Tanzania bara iliyokuwa na mikutano 247 na kupokea kero zaidi ya 2000 ambazo zimebainisha mambo matatu ikiwemo Dhulma ilioyokithiri katika ardhi,Biashara na viongozi kutotatua kero za wananchi na ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Makonda amewaleza wanahabari jijini,Dar es Salaam kuwa timu yake inaandaa ripoti ili kumkabidhi Katibu mkuu na baadae mwenyekiti wa Chama ili kuona matatizo yanayowakabili wananchi na namna ya kuyatatua katika baadhi ya maeneo ambayo wamekutana na wananchi ingawa matatizo mengine yanaweza kuchukuwa muda kutatuliwa kutokana uhitaji wa mabadiliko ya kimfumo na kisheria.
Amesisitiza kuwa Chama cha Mapinduzi kina misingi ya utawala wa sheria usiohitaji dhulma hivyo wamemugiza Waziri wa Ardhi kuweka utaratibu wa kukutana na wananchi ili kuondoa dhulma iliyotamalaki katika ardhi inayofanywa na wanamtandao wanaoshirikiana na watumishi wasiokuwa waaminifu.”unakuta eneo moja hati juu ya hati,nani ametoa?amechukuliwa hatua gani? amehoji.
Aidha katika maeneo ya biashara baadhi ya wananchi wamedhulumiwa fedha zao na bila ya kubaki na vielelzo vya madai yao kutokana na udanganyifu uliotumika kwa upande wa wakulima wengine wa mahindi mkoani Ruvuma wamedhulumiwa Shilingi bilioni 7 kutoka kwa wanunuzi wa mazao.
Utaratbu wa kukutana na Rais kila mwisho wa mwezi utatolewa wakati wowote kuanzia sasa,ambapo wananchi wanaotakiwa kukutana nae ni wale ambao wameishapeleka kero zao katika ngazi husika kulingana na kero hizo na bado hazipatiwa majibu kwa muda mrefu.