Sat. May 16th, 2026
  • Wamkabidhi tunzo ya shukrani Said Salim Bakhresa kwa ujenzi wa klabu yao

Klabu ya Pan African ya jijini Dar es Salaam imefanya dua maalum kwa ajili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, siku moja baada ya kuchukua fomu ya kugombea urais, wakimuombea ushindi na uwezo mkubwa wa kuongoza nchi katika kutatua changamoto za maendeleo.

Dua hiyo imefanyika katika makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo Mtaa wa Swahili, Kariakoo, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Ujenzi, Ndugu. Abdallah Ulega, na Waziri wa Mambo ya Nje, Ndugu Balozi Mahmoud Thabiti Kombo pia imetumika kama sehemu ya kuwaombea wachezaji na wanachama wengine ambao wamefariki dunia akiwemo muasisi wa klabu hiyo ndugu, Mangara Tabu.

Uongozi wa klabu hiyo,chini ya Mwenyekiti wake, Ndugu Adam Kirumbi wametumia maombi hayo pia kutambua michango mbalimbali iliyotolewa katika kuendeleza klabu hiyo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa jengo la klabu lililojengwa na mfanyabiashara maarufu Said Salim Bakhresa.

Hitma hiyo pia iliambatana na utoaji wa tuzo kwa wanachama na wapenzi wa mpira wa miguu waliowahi kuipeperusha vyema bendera ya Pan African Sports Club. Wachezaji wa zamani waliotunukiwa tuzo kwa pamoja ni Sunday Manara, Juma Pondamali, Mohamed Richard Aldof, na Carlos Mwinyimkuu, na wenzao ambao walikumbukwa kwa mchango wao katika mafanikio ya klabu.

Pondamali ‘aponda’ makipa wa kigeni

Klabu ya Pan African iliwahi kushiriki mashindano makubwa barani Afrika, ikiwemo Klabu Bingwa Afrika na Kombe la Shirikisho katika miaka ya 1980, ikibaki kuwa moja ya timu zenye historia kubwa katika soka la Tanzania.