Sun. Jun 15th, 2025
Wawakilishi wa mashirika ya Umoja wa mataifa wakizungumza na waandishi wa habari ofisini kwao Kinazini kushoto ni Leila Miraji Kihwele wa FAO, Dr Maryam Seif Hamad wa UNICEF, Mratibu wa ofisi ndogo za Umoja wa Mataifa UN Zanzibar Dorothy Temu Usiri, Ali Haji Hamad wa UNFPA na Elizabeth Masurulu wa UNOPS

Jamii inapaswa kupata haki ya afya ya uzazi,uwezeshaji wa wanawake na wasichana ili kuweka mazingira endelevu kwa kutatua changamoto mbalimbali zinazowzakabili kulingana na kutokuwepo kwa ulinganifu katika usawa wa kijinsia.

Kundi la wanawake na wasichana wanapitia matatizo ya afya ya uzazi kutokana na kutokuwepo kwa mabadiliko chanya ya ustawi wa jiamii.

Afisa wa program za jinsia za shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani,UNFPA Ali Haji Hamad ameeleza juu ya masuala mbalimbali kama hatua za kuondoa changamoto zinazowakabili wanawake,afisini kwake Kinazini Unguja,ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Umoja wa Mataifa.

Amesema jamii inapaswa kuwekewa mazingira mazuri ili kuhakikisha wanaondokana na changamoto zinawakabili sambamba na kuwa na mikakati itayosaidia kuweka mazingira endelevu kwa jamii.

Amefahamisha kuwa UNFPA inafanya kazi katoka maeneo manne muhimu ili kutimiza azma ya Serikali ya Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Ametaja maeneo hayo kuwa ni pamoja na huduma za afya ya uzazi wa mpango, pasiwepo vifo vya uzazi vinavyoweza kuzuilika, pasiwepo na udhalilishaji na ukatili wa kijinsia na pasiwepo na maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi.

Akitoa salam za Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mratibu wa ofisi ndogo za Umoja wa Mataifa UN Zanzibar Dorothy Temu Usiri amesema umoja huo unajivunia mafanikio kumi ya kutoa huduma duniani kote.

Baadhi ya mafanikio hayo ni pamoja na kusaidia na kulinda watu milioni 131 duniani wanaokimbia vita, njaa na mateso, kutoa chakula na usaidizi wa watu  zaidi ya milioni 150 katika nchi na maeneo zaidi ya 120 duniani.

Mwakalishi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto dunian, UNICEF Dr Maryam Seif Hamad ameeleza kuwa ushirikiano na serikali unatoa usaidizi katika sekta za afya, elimu, maji safi, hifadhi ya mtoto na usafi wa mazingira ili kukuza ustawi wa mtoto hapa nchini.

Umoja wa mataifa huadhimisha siku ya Umoja huo kila ifikapo Oktoba 24 ya kila mwaka ambapo ujumbe wa mwaka huu ni Ustawi wa vizazi vijavyo kuendesha ukuaji endelevu.