Sun. Jun 15th, 2025

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) inapenda kuwatangazia wadau wake hususan madereva wa gari za wageni na waongoza watalii (Tour Guides) kuwa, baadhi ya barabara ndani ya Hifadhi hiyo zitafungwa kwa muda kwa ajili ya matengenezo kutokana na athari za kujaa maji na barabara zingine kuharibiwa na mafuriko ya mvua zinazoendelea kunyesha.

Kaimu meneja wa uhusiano kwa Umma wa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro(NCAA) ameeleza kuwa barabara zitakazofungwa kwa muda kuanzia tarehe 27 aprili, 2024 ni pamoja a barabara ya Ngoitoktok kuelekea msitu wa Lerai kupitia mifupa ya tembo, barabara kutoka msalaba mkubwa kwenda msitu wa lerai kupitia vumbi la Kongoni, Barbara kutoka Ngiotoktok picnic Site kuelekea maeneo maalum ya kulishia wageni (Bush Lunch) a barabara ya Viboko (Hippo Pool).

Barbara nyingine itakayofungwa kutokana na athari ya mafuriko ni barabara kutoka Kijiji cha Endulen kuelekea tambarare za dutu kupitia Mlima Matiti, aidha eneo la tambarare a Ndutu sehemu kubwa ya ardhi imeshiba maji, hivyo madereva wanashauriwa kutochepuka pembeni mwa barabara kuepuka gari za wageni kukwama.

Katika taarifa yake kwa Umma ndugu Hamis amesisitiza Madereva kuwa makini katika barabara ya Seneto kuelekea Bonde la Ngorongoro (entry road) a barabara ya kupanda kutoka Kreta ya Ngorongoro (Exit Road) ambapo kutokana na ardhi kushiba maji wakati mwingine husababisha maporomoko ya udongo barabarani.

Timu yetu ya wataalam wa Uhandisi inaendelea na kazi ya kurekebisha maeneo yote yaliyoathirika a mvua zinazoendelea kunyesha ili kurejesha huduma katika maeneo yote yaliyoathirika.