Benki Kuu ya Tanzania haitambui taasisi, kampuni na watu binafsi
wanaojitangaza kuwa mawakala au washauri elekezi (consultants) wanaotoa huduma ya
kusaidia waombaji kupata leseni au usajili wa watoa huduma ndogo za fedha, maduka ya
kubadilisha fedha za kigeni, benki na taasisi za fedha, watoa huduma za mifumo ya malipo,
na watoa huduma za fedha kupitia mitandao ya simu zinazosimamiwa na Benki Kuu.
Aidha, Benki Kuu imebaini kuwa baadhi ya matangazo yanayotolewa na washauri hao sio sahihi kulinganisha na gharama zinazohusika. Hivyo Benki Kuu inasisitiza waombaji kutafuata gharama hizo kjutoka katika ofisi zao ili kujiepusha na watu wasio waaminifu.Sheria ya Fedha za Kigeni ya mwaka 1992, Sheria ya Benki na Taasisi za
Fedha ya mwaka 2006, Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018 na Sheria ya
Mifumo ya Malipo ya Taifa ya mwaka 2015 na kanuni zake zimeainisha viwango vya mitaji
na gharama za maombi ya leseni ya kila aina ya taasisi. Gharama ya maombi ya leseni,
ambazo hulipwa moja kwa moja katika akaunti ya Benki Kuu,