Sun. Jun 15th, 2025
Baadhi ya watalii wakiwa katika hifadhi ya Ngorongoro kushuhudia vivutio

Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro (NCCA) imesema shughuli za utalii katika hifadhi hiyo zinaendelea kama kawaida licha ya kuripotiwa maandamano ya amani kwa baadhi ya wananchi wanaoishi katika hifadhi hiyo.

Kaimu meneja,kitengo cha uhusiano kwa Umma Bw, Hamis Dambaya ameeleza kuwa watalii kutoka ndani na nje ya Tanzania wanaendelea na safari zao kama ilivyokuwa awali katika kushuhudia vivutio vya utalii ndani ya hifadhi na Serikali inaendelea kuhakikisha usalama wao.

Mitandano mbalimbali ya kijamii ilionesha baadhi ya wananchi wanaoishi katika hifadhi hiyo wakiongea na baadhi ya watalii wakiwa na mabango yenye ujumbe tofauti unaosisitiza juu ya haki za binadamu.

Serikali kupitia Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro imekuwa ikitoa elimu juu ya uhamaji wa hiari katika hifadhi hiyo ili kupunguza shughuli za kibinadamu zinazoweza kuathiri kwa kiasi kikubwa mazingira na wanyama hifadhi ya Ngorongoro.