Sat. Jun 14th, 2025

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Tanzania Bara utafanyika kwa wagombea wa nafasi mbalimbali ikiwemo za Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa,Mwenyekiti wa kijiji,Mwenyekiti wa Kitongoji,wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (kundi mchanganyiko la wanawake na wanaume) na wajumbe wa Halmashauri ya kijiji(kundi la wanawake), wenyeviti wa vitongoji katika mamlaka za wilaya baada ya wanachama kuidhinishwa na vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu.

Waziri wa ncjhi,ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Seriikali za Mitaa Mhe Mohamed Mchengerwa(Mb) ametangaza uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mujibu wa kanuzi za uchaguzi za mwaka 2024 chini ya mamlaka za Serikali za Mitaa ngazi ya vijiji,vitongoji na mitaa katka Mamlaka katika za Wilaya na Mamlaka za Miji.

Zoezi la uchukuaji na urudishaji wa fomu za wagombea ni kati ya tarehe 1 hadi 7 Novemba huku uteuzi wa wagombea ukifanyika tarehe 8 Novemba ukifuatiwa na mapingamizi ya uteuzi kulingana na wagombea husika kabla ya kuanza kwa kampeni za uchaguzi huo.Taarifa ya Waziri Mohamed imesisitiza kuwa uandikishaji na uandaaji wa orodha ya wapiga kura utaanza siku ya arobaini na saba kabla ya siku ya uchaguzi na utafanyika kwa muda wa siku kumi tu ukifatiwa na muda wa mapingamizi kwa wapigakura.

Vyama vya Siasa 19 ndio vina usajili wa kudumu kwa mujibu wa orodha ya msajili wa vyama vya Siasa nchini,huku chama tawala,Chama cha Mapinduzi kikipewa nafasi kubwa dhidi ya vyama vya upinzani kama Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema),Chama cha Wananchi(CUF),ACT Wazalendo kulinganisha na mitandao ya wanachama wao na wapigakura kwa ujumla.