Mtoto wa aliyekuwa Waziri Mkuu,Mstaafu hayati,Edward Moringe Sokoine,ndugu Namelock Edward Sokoine amechaguliwa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa(NEC) kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa.
Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halamashauri Kuu ya CCM Taifa,Itikadi,Uenezi na Mafunzo,Ndugu Amos Gabriel Makalla imeeleza kuwa waliochaguliwa pamoja na Namelock Sokoine ni Dkt Juma Abdallah(Mabodi),Ndugu Salim Faraj Abri(Asas), na Ndugu Hamad Hassan Chande.