Serikali imetoa ufafanuzi kuhusu malalamiko ya madai ya kutotendewa haki kwa baadhi ya wananchi waliohama kwa hiyari katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro kwenda katika makazi mapya ya kijiji cha Msomera wilayani Handeni,mkaoni Tanga.
Malalamiko hayo yamekuja baada ya wananchi 132 kati yao ni wategemezi katika kaya zilizolipwa baada ya kufanyiwa tathmini na kujaza fomu mbalimbali ambazo zimeonyesha wakuu wa kaya waliolipwa kwa niaba yao.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni mkoani,Tanga, Ndugu Albert Msando amesema serikali haitoruhuisu mtu yoyote kufanya vitendo vya utapeli ama udanganyifu katika mradi wa kuhamisha wananchi kwa hiari kutoka katika hifadhi ya Ngorongoro kwenda katika Kijiji cha Msomera kilichopo wilayani humo.
Mazungumzo na wanahabari katika Kijiji cha Msomera,hivi karibuni amesema amefika katika Kijiji hicho ili kukutana na mwananchi yoyote ambaye anaamini hajatendewa haki wakati wa kuhama kutoka katika hifadhi ya Ngorongoro kwenda Kijiji cha Msomera ili aweze kutatua changamoto yoyote kuhusiana na madai hayo.
“Wananchi 132 ambao waliorodhesha majina yao na kuyaleta kwangu niliyatuma majina hayo Mamlaka ya Hifandhi ya Ngorongoro,na serikali imegundua kuwa watu hao hawakuwa wakuu wa kaya wakati wanahama kuna watu wanataka kuleta utapeli katika zoezi hili na wengine wapo nchi za nje wakiamini kwamba kuna fedha za bure ili wafanye utapeli,hilo halikubaliki na ndio maana leo nimekuja tena hapa kama wana jambo lolote la ziada”
Kuhusu wananchi watatu ambao majina yao yameongezeka katika taarifa iliyotolewa na baadhi ya vyombo vya Habari,Ndugu Albert amesema vyombo husika vinafuatilia madai hayo ili kuona kama yana ukweli.
Mkuu huyo wa wilaya amesisistiza kuwa zoezi la kuhamisha watu kutoka ndani ya hifadhi ni la hiyari na ndio maana wahusika wote wanahusishwa kuanzia hatua ya uelimishaji,uandikishaji, na uhamishaji wa wananchi na mali zao ambapo kila mwananchi anaekubali kuhama husaini fomu mbalimbali zinazomuwezesha kupata stahikio zake kwa haraka.
Jumla ya wananchi 132 ambao wategemezi wa kaya zilizohama kwa hiari kutoka ndani ya hifadhi ya Ngorongoro kwenda katika Kijiji cha. Msomera walilipotiwa na baadhi ya vyombo vya Habari wakidai kuwa Serikali haijawapa stahiki zao wakati wa zoezi la kuhama kutoka katika hifadhi.
Awamu ya kwanza serikali ilijenga nyumba 503 katika kijiji cha msomera na kaya 551 kuhamia zikiwa na watu3,010 na mifugo 15,521.