Mchezo wa pili fainali ya ligi ya Shirikisho Barani Afrika unazikutanisha tena timu za RS Berkane na Zamalek ya Misri,utachezwa siku ya Jumapili jijini Cairo,huku timu ya Zamalek ikiwa imepoteza mchezo wa kwanza kwa kufungwa goili 2-1 huko Morocco.
Fainali hiyo itakuwa ya kuvutia zaidi kulingana na ubora wa vilabu hivyo kuwa na wachezaji wenye uwezo mkubwa kama vile Ahmed Mustafa Zizo ambae anacheza nafasi ya wingi ya kulia inayomuzesha kutengeneza mashambulizi yenye madhara na Omar Jober ambae ni beki wa kulia mwenye uwezo mkubwa wa kupandisha mipira yenye madhara kwa upande wa timu ya Zamalek Huku timu ya RS Berkane ikiwategemea nyota wake Dayo Issoufou ambae anacheza nafasi ya kati katika kuzuia mashambulizi akisaidiana na Yassine Labahiri anacheza kama kiungo mshambuliaji.
Hii ni fainali ya pili kuwakutanisha RS Berkane na Zamalek ambayo fainali ya kwanza ilikuwa mwaka 2019 ambapo ilianzia Morocco na mchezo wa pili kufanyika Cairo,Misri.
