Sun. Jun 15th, 2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Samia Suluhu Hassan ataongoza ibada ya kumuombea hayati Waziri Mkuu mstaafu wa tatu katika serikali ya awamu ya kwanza Bw Edward Moringe Sokoine katika kumbukizi ya kuenzi masuala mbalimbali aliyowahi kufanya kuanzisha dira ya mifugo,kujitosherza katika kilimo.

Msemaji wa Familia,Bw Lembrika kipuyo amewaambia waandishi wa habari jijini Dodoma kuwa suala la kilimo si la kubeza kwa kuwa nia ya kilimo ni kusaidia nchi katika uchumi wa Taifa,hivyo Mh Edward alilisistiza Elimu,afya na mazingira pamoja na vyanzo vya maji ili kusaidia kilimo cha kisasa na kilimo biashara Wakati wa uhai wake alisimamia uanzishwaji wa sera ,mabwawa ya maji na madawa ya mifugo

Waziri Mkuu wa Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aliwahi kuwa Waziri Mkuu mara mbili, tangu tarehe 13 Februari, 1977 hadi 7 Novemba, 1980  na mara ya pili kuanzia tarehe 24 Februari, 1983 hadi tarehe 12 Aprili, 1984 alipofariki kutokana na ajali ya gari baada ya kugongana na gari aina ya Landcruiser lililokuwa likiendeshwa na mpigania uhuru wa chama African National Congress (ANC) Domisani Dube (23) lilokuwa likiendeshwa katika eneo la Dakawa mkoani Morogoro akitokea Dodoma mwaka 1983.