Sun. Jun 15th, 2025
  • JNHPP 33% hadi 96.28%,umeme kuuzwa Uganda,Kenya,Ethiopia,Sudan Kusini,Sudan na Zambia
  • Reli ya kisasa(SGR) Dar hadi DRC,Uganda,Rwanda,Burundi
  • Meli 4,318 Machi 2021 hadi Meli 4762 Feb 2024, shehena tani mil 17,287 hadi mil 26.544, 2024
  • 2021/4 barabara 57 zenye urefu wa km 3,794.1,Madaraja 8 likiwepo daraja la Magiufuli katika utekelezaji chini ya Tanroads
  • bajeti ya elimu trilioni 4.72 hadi trilioni 5.98 mwaka 2023/24
  • Watalii kutoka 922,692 hadi 1,808,205 wameingiza dola za Marekani bilioni 3.37
  • Serikali imekoa bilioni 860.6 baada ya kushinda kesi
  • Tanzania yashika nafasi ya pili Africa kwa ubora wa usalama mtandaoni

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Samia Suluhu Hassan ameelekeza kujengwa kwa reli itakayozifika nchi jirani za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,Burundi,Rwanda na Uganda ili kuyafikia masoko ya kikanda katika kukuza biashara na uchumi wa nchi kwa kuzingatia pato la Taifa.

Serikali inafanya ununuzi wa treni za Kisasa (EMU) SETI 10;Mabehewa ya abiria 89;na mabehewa ya mizigo 1,430 kwa hthamani ya dola za Kimarekani milioni 506.6 sawa na shilingi trilioni 1.2

Msemaji wa Serikali,Bw Mobhare Matinyi ameeleza jijini,Dar es Salaam wakati akibainisha masuala mbalimbali ya Serikali ikiwemo ujenzi wa awamu ya pili wa reli ya SGR ulioanza kwa vipande vya kutoka Tabora hadi Kigoma (km 506) huku Uvinza hadi Msongati (km 367) taratibu za manunuzi zikiwa zinaendelea .

Aidha Serikali imeboresha na kujenga magati katika badari za Dar es Salaam,Mtwara na Tanga pamoja na maeneo ya maziwa makubwa pamoja na kuweka vifaa vya kisasa ili kuongeza shehena za magari na mizigo mchanganyiko.

Vinginevyo Bw Mobhare amesema katika kipindi cha Serikali ya awamu ya Sita chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan,Mamlaka ya kukusanya Kodi nchini(TRA) ilivunja rekodi ya ukusanyaji ambao ulifanyika kwa maelewano baina ya walipa kodi na Mamlaka hiyo na kufikia kiwango cha trilioni 3.5 kwa mwezi Disemba 2023 huku mfumuko wa bei ukizikidi kushuka na kufikia kiwango cha chini ya 4%

Sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi ya mwaka 2022 imeifanya nchi kushika nafasi ya pili barani Afrika kwa ubora wa usalama mtandaoni kwa mujibu wa ripoti ya Global Cybersecurity Index(GCI)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *