Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejiandaa kuwasilisha andiko la kitaalamu ili kuonba idhini kwa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ili kupata idhini ya kutengeneza miundombinu ya barabara kwa tabaka gumu katika hifadhi ya Serengeti kutokana na uharibifu uliosababishwa na mvua kubwa katika kipindi cha mwezi Oktoba 2023 hadi machi 2024.
Licha ya kuwepo kwa changamoto ya mvua kubwa lakini Idadi ya watalii imefikia 1,451,176 hadi kufikia mwezi februari mwaka huu ukilinganisha na kiwango cha makadirio ya kuwa na watalii 1,387,987 yaliyowekwa kwa mwaka wa fedha 2023/24 katika hifadhi zote 21 zilizo chini ya Shirika la hifadhi la Taifa (Tanapa).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw Mobhale Matinyi alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dodoma ametaja ongezeko la watalii nchini limetokana na filamu ya Royal Tour iliyomhusisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Samia Suluhu Hassan.” Idadi ya Watalii wanaokuja Serengeti sasa imekwenda juu kupita malengo makubwa yaliyowekwa katika mwaka huu wa fedha” ameongeza.
hifadhi ya Taifa ya Serengeti imeshinda Tuzo ya Hifadhi bora Afrika kwa miaka mitano mfululizo ambayo inachochiowa na umaarufu wa zaidi kwa tukio la kuhama kwa wanyama aina ya nyumbu 1.5 ambao hutumia miezi kumi kuzungunga na kwenda nchi jirani na kisha kurejea baada ya kuvuka mto Mara.
hifadhi ya Serengeti ilianzishwa mwaka 1959 kwa ukubwa wa eneo la kilomita za mraba 14,763 ndio hifadhi ambayo mtalii anaweza kuona wanyama wote watano maasrufu,yaani Simba,Chui,Tembo ,Nyati na Kifaru.