Rais wa Young Africans SC na Mwenyekiti wa vilabu vya Soka Barani Afrika (ACA) Mhandisi Hersi said Desemba 5, 2023 ametembelea eneo la mafuriko katika kijiji cha Katesh wilaya ya Hanang Mkoani Manyara na kutoa pole kwa waathirika wote wa mafuriko hayo.
Akiunga mkono wito wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu_Hassan, klabu ya Yanga kwa kushirikiana na GSM Foundation imechangia vitu vyenye thamani ya Tshs. 40,000,000 pamoja na fedha taslim Tshs. 10,000,000 kupitia Akaunti ya Mfuko wa Taifa wa Usimamizi wa Maafa.
Msaada huo ulipokewa na Mhe. Jenista Mhagama Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) akiambata na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh. Queen Sendiga pamoja na viongozi mbalimbali waliokoKatesh kusaidia zoezi zima la uokozi.
