
Simba Queens yabeba Ngao ya Jamii 2023

Timu ya Simba Queen imechukua Ngao ya Jamii 2023 kwa wanawake katika mchezo uliomalizika kwa timu ya JKT Queens kufungwa jumla ya magoli 6-5 na Simba Queens klatika mchezo uliochezwa katika uwanja wa chamanzi complex nje kidogo ya jiji la Ilala mkoani Dar es Salaam.
Michezo huo uliochezwa Disemba 12, 2023 ulimalizika kwa timu za JKT Queen na Simba Queen kupata sare ya magoli 1-1,ambapo mwamuzi wa mchezo huo aliamua kupigwa kwa penati zilizoipatia ushindi Siimba Queen magoli 5-4 dhidi ya JKT Queen.
Wizara ya Michezo kujenga viwanja vya michezo Dododma
.jpg)
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Gerson Msigwa amesema Jengo jipya la Wizara hiyo linalojengwa katika mji wa Serikali Mtumba litakua na eneo la michezo na burudani katika eneo la mbele la jengo hilo,ili kuakisi dhima ya Wizara hiyo ya kukuza na kuendeleza Utamaduni, Sanaa na Michezo hapa nchini.
Katibu Mkuu Msigwa amesema hayo Desemba 13, 2023 alipofanya ukaguzi wa maendeleo ya Ujenzi wa jengo hilo, ambapo amesema tayariameshauriana na Mkandarasi pamoja na Mshauri elekezi wa Jengo hilo wafanye maboresho madogo katika eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya maegesho ya magariliwe eneo la viwanja vidogo vya mpira wa miguu, kikapu na netiboli.
“Nimetembelea mradi, nimeona kazi inaendelea vizuri na sasa tupo asilimia 74, na kwa maelekezo ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa lazima tuingie kwenye jengo hili mwezi Januari mwaka 2024, kwahiyo
kama wizara tunaendelea kuhakikisha kazi inafanyika usiku na mchana ili Januari tuhamie” amesisitiza Katibu Mkuu Msigwa.
Amesema vifaa vyote kwa ajili ya kumaliza kazi iliyobaki vimeshawasili eneo la mradi hivyo Mkandarasi ambaye ni Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) anatakiwa kuhakikisha kazi inafanyika kwa haraka na ubora.
Kwa upande wa Mshauri Mwelekezi wa Mradi pamoja na Meneja Mradi wamesema watazingatia ushauri na maelekezo ya Katibu Mkuu huku wakiahidi kukamilisha kazi zilizobaki kwa wakati.
Tanzania yatolewa mashindano ya CAF
Timu za Tanzania zimetolewa katika mashindano ya mpira wa miguu kwa wavulana na wasichana chini ya miaka 15 yanayojulikana kuwa African school football champioship yanayosimamiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani afrika(CAF),huko visiwani Zanzibar.
Mashindano hayo ambayo yamefikia hatua ya fainali ambayo itaanza kuchezwa tarehe 21 hadi 24 Mei mwaka 2024 yameshirikisha nchi 44 kutoka Barani afrika ambapo jumla ya wachezaji wa kiume 804,480 na vijana wa kike 28,862 ikiwa ni ongezeko la 40% ukilinganisha na mashindano yaliyopita.
Timu 12 zilizofuzu fainali za mashindano hayo kwa upande wa wavulana ni pamoja na Benin,Libya,Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo,Senegal,South Afrika na Uganda ambapo kwa wasichana ni Gambia,Morocco,Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo,South Afrika,Togo na Uganda.
Mshindi wa mashindando hayo atapata fedha taslimu Dola za Kimarekani 300,000 kwa upande wa wavulana na wasichana,wakati mshindi wa pili atajinyakulia fedha taslimu kiasi cha Dola la Kimarekani 150,000.Zawadi hizi zitaambatana na mpango maalum wa kuendeleza mpira wa miguu unaotolewa na Taasisi ya Motsepe (Motsepe Foundation).
Kabla ya mashindano hayo shirikisho kla Soka barani afrika (CAF) liliendesha mafunzo ya ukocha yenye hadhi ya leseni D,Mafunzo ya huduma za kwanza,mafunzo ya utoaji wa taarifa.
