Ukurasa huu ni kwa ajili ya kuelekeza wasomaji wetu jinsi kupata huduma zinazotolewa na taasisi na Wakala mbalimbali za Serikali hasa katika usajili na maelekezo yake Tanzania Bara.
Tunaanza na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni(BRELA)
Hatua ya kwanza;
Andika neno; www.brela.go.tz kwenye kibox cha utafutaji tovuti kama ifutavyo:

Baada ya hapo ukurasa wa Wakala wa Usajili wa Biashara na leseni utafunguka kama unavyoonekana hapo chini.

Huduma zinazotolewa na Brela

Kabla ya kuchagua aina ya usajili unaotaka,tafadhari bonyeza sehemu iliyoandikwa mifumo ili ufungue akaunti yako itakayotumika kuwasiliana na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni(BRELA).Pia hakikisha una taarifa zako muhimu kama Tarehe ya kuzaliwa,Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au namba zake,anuani ya barua pepe(E-mail)

Bonyeza neno Mifumo,utaona maneno yafuatayo:
- Mfumo wa Usajili wa ORS
- Mfumo wa leseni za Biashara
- Mfumo wa Taarifa za Kimataifa
- Mfumo wa Wamiliki Manufaa
Chagua na bonyeza neno; Mfumo wa Usajili wa ORS utaona kiboksi cha rangi ya njano kimeandikwa “Tengeneza akaunti ya ORS“.Bonyeza hicho kiboksi.

Jaza taarifa zako zinazohitajika katika fomu hii kwa kuangalia mfano wa ujazaji kisha jaza kwa kutumia tovuti ya BRELA ili upate akauti yako itakayotumika kutunza maelezo yako na kuitumia pindi unapowasiliana na Msajili kulingana na huduma husika.
